Numbers 27:12-17

12 aKisha Bwana akamwambia Musa, “Panda juu ya mlima huu katika kilele cha Abarimu uione nchi ambayo nimewapa Waisraeli. 13 bBaada ya kuiona, wewe pia utakusanywa pamoja na watu wako kama ndugu yako Haruni alivyokusanywa, 14 ckwa kuwa jumuiya ilipoasi amri yangu kwenye maji katika Jangwa la Sini, wakati jumuiya ilipogombana nami, nyote wawili mliacha kuitii amri yangu ya kuniheshimu kama mtakatifu mbele ya macho yao.” (Haya yalikuwa maji ya Meriba huko Kadeshi, katika Jangwa la Sini.)

15Musa akamwambia Bwana, 16 dBwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii 17 eili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”

Copyright information for SwhKC